The House of Favourite Newspapers

Sokabet Beach Soccer Sasa Kufanyika Coco

0
Beach Soccer likiendelea.

MICHUANO ya Beach Soccer inayodhaminiwa na gazeti namba moja la michezo Tanzania la Championi na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha Matokeo, Sokabet, inatarajiwa kuendelea kesho na keshokutwa Jumapili kwa timu mbalimbali kuchuana.

Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu 16 za vyuo mbalimbali hapa nchini, itahamia kwenye fukwe za Coco, Masaki ikitokea Escape One jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa ratiba za mechi za kesho Jumamosi, DSJ watafungua pazia la michuano hiyo kwa kuvaana na Tumaini saa mbili kamili asubuhi.

Mechi nyingine zitakazofuata ni DIT vs HKMU (saa 3:00), NIT vs UAUT (saa 4:00), LBC vs Ardhi (saa 5:00) zote asubuhi na MNMA vs CBE (saa 6:00), MCET vs TIA (saa 7:00) zote mchana.

Nyingine ni SIBM vs TPSC (saa 8:00), DMI vs IFM (saa 9:00 alasiri) na Ardhi vs HKMU (saa 1:00) kabla ya kumalizia mchezo wa mwisho Tumaini vs UAUT (saa 11:00) zote za jioni. Michezo ya Jumapili; DMI vs AMCET ambazo zitaanza kucheza saa mbili kamili asubuhi, michezo mingine ya asubuhi ni DIT vs NIT (saa 3:00), SIBM vs TIA (saa 5:00).

Michezo ya mchana siku hiyo itakuwa ni DSJ vs HKMU (saa 6:00), MNMA vs IFM (saa 7:00), LBC vs UAUT (saa 8:00) kabla ya saa 9:00 alasiri kucheza TPSC dhidi ya CBE. Timu nyingine zitakazocheza siku hiyo ni; Ardhi vs Tumaini (saa 10:00) kabla ya TPSC kucheza na IFM saa 11:00 jioni.

Wilbert Molandi, Championi.

Matukio kama haya na mengine, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

 

Spoti Hausi LIVE: Selemani Matola Alivyoikazia Simba SC

Leave A Reply