The House of Favourite Newspapers

Solskjaer Man United walicheza kama enzi za Mourinho

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amewaponda wachezaji wake kwa kuwaambia walicheza kama alivyokuwa anawafundisha Jose Mourinho, wikiendi iliyopita.

 

Kocha huyo aliishuhudia United ikipoteza mchezo muhimu wa Kombe la FA dhidi ya Wolves walipochapwa mabao 2-1 na kuondolewa kwenye michuano hiyo. Baada ya mechi hiyo, kocha huyo alisema kuwa timu yake ilicheza vibaya kuliko kipindi kingine chochote kile ambacho amekuwa akiifundisha.

Kocha huyo amesema kuwa timu hiyo ilionekana kurudi kwenye enzi za Mourinho ndiyo maana ikapoteza mchezo huo muhimu kwao. Inaelezwa kuwa Solskjaer akiwa vyumbani aliwaambia wachezaji wake kuwa hawakufuata maelekezo yake kwenye mchezo huo na walikuwa wakicheza kama enzi za Mourinho.

“Mlirudi sana nyuma, hiki ni kiwango cha chini zaidi ambacho nimekuwa nikikiona kwenye timu hii, najua kuwa tulicheza vizuri kwenye mechi dhidi ya Arsenal, lakini  tukapoteza, lakini kwenye mchezo huu tulishindwa kufanya vizuri kwa kuwa hatukufuata maelekezo.

 

“Mnakwenda kwenye kipindi cha wiki mbili cha timu ya taifa na wengine mnaendelea na maandalizi ya ligi na vizuri mkatumia nafasi hiyo kutafakari kama kweli mlikuwa sahihi,” alisema kocha huyo ambaye timu yake ipo robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Comments are closed.