The House of Favourite Newspapers

Ole Gunnar Solskjaer Naitaji Ubingwa Man United

Ole Gunnar Solskjaer

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema yeye mawazo yake siyo kumaliza kwenye nne bora mwishoni mwa msimu bali kutwaa kombe.

 

United kwa sasa ipo kwenye kasi nzuri ikiwa ipo kwenye makombe matatu makubwa, Kombe la FA, Ligi Kuu England pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kocha huyo amesema kuwa anaona kuwa timu yake inaweza kutwaa ubingwa wowote msimu huu na hivyo yeye anawaza makombe. Amesema kama wataweza kuingia kwenye nne bora lakini wakashindwa kutwaa makombe, haiwezi kuwa jambo zuri kwake.

 

“Nne Bora siyo jambo la mafanikio kwangu, sisi ni Manchester United lazima tuwe na dhamira ya kutwaa makombe sana sana lile la ligi.

 

“Siyo lazima msimu huu bali tunaweza kufanya hivyo msimu ujao, tupo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na FA na tunaona kuwa tunaweza kufanya vizuri huko,” alisema kocha huyo wa muda.

Comments are closed.