The House of Favourite Newspapers

Soma Msimamo wa CCM Kuhusu Mikopo Kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu

0

Siku chache baada ya Mbunge wa Bunda Vijijini (CCM), Mwita Getere kutoa hoja bungeni iliyozua mjadala mzito akipendekeza Wanachuo waondolewe pesa ya kujikimu ‘Boom’ kwa kuwa wanaitumia vibaya akidai wanalewa tu pombe, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa msimamo wake kwa kupinga kauli hiyo.

“Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuwajulisha wadau wote wa elimu na Umma wa Watanzania kuwa kitaendelea kuisimamia Serikali ili kuongeza utoaji wa mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu wenye sifa stahiki.

…Kadhalika, Serikali ya CCM imeongeza pesa ya kujikimu, ‘boom’ toka Tsh 8,500/- hadi Tsh 10,000/- kwa siku.

Tunauhakikishia Umma wa Watanzania kuwa CCM itaendelea kuisimamia Serikali kutenga na kutoa pesa hizi za kujikimu na gharama nyingine kwa wanufaika wengi zaidi wenye sifa stahiki.

Maoni ya baadhi ya watu juu ya kuondolewa kwa fedha za kujikimu hayatazingatiwa kwani hakuna haja ya kumpangia matumizi ya fedha mtu mzima.

CCM itaendelea kupokea maoni ya namna bora ya kuboresha na kuimarisha mikopo hii.

Serikali ya CCM haina mpango wa kufuta au kuondoa mikopo hiyo kwani ina tija kubwa, kwa kutoa nafasi hasa kwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia zisiÄ°zoweza kugharimia Elimu ya Juu, kusoma vyuo vikuu hapa nchini.

Aidha, tunawahakikishia wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu kuwa Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kubeba matarajio na maslahi yao kwa namna ya kipekee.” – Chama Cha Mapinduzi.

Leave A Reply