The House of Favourite Newspapers

Songea: Washindi wa Mdahalo kwa Shule za Sekondari Watunukiwa

0

1    Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya De Paul wakiwa na tuzo za IPad na ngao ya dhahabu baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (Jica), Toshio Nagase (kulia) pamoja na mjumbe wa kamati kuu ya shirika hilo, Jacob Katanga. Jica ndiyo imedhamini tuzo hizo katika mdahalo uliyoratibiwa na Tamasha la Majimaji Selebuka.

2Wajumbe wawakilishi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (Jica) ambalo limedhamini zawadi za IPad kwa shule tatu zilizoibuka kidedea kwenye mdahalo kwa shule sekondari mkoani Ruvuma ulioratibiwa na Tamasha la Majimaji Selebuka. Kutoka kushoto ni Kei Umetsu, Zuhura Mwakijinja (Afisa miradi), Toshio Nagase (Mkurugenzi) na Jacob Katanga.

3Mwanachama wa Jata ambacho ni chama katia Shirika la Jica, Dk Damas Ndumbaro akitoa hotuba kwa wanafunzi wa shule za De Paul, Chipole na Songea Girls zilizoibuka kidedea katika mdahalo kwa shule za sekondari ulioratibiwa na Tamasha la Majimaji Selebuka. Mdahalo huo umefanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea.

4Wanafunzi wa shule za De Paul, Chipole na Songea Girls wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutunukiwa zawadi za IPad na ngao kwa kuibuka kidedea kwenye mdahalo ulioshirikisha jumla ya shule 11 za shule za sekondari za Mkoa wa Ruvuma. De Paul ndiyo bingwa, ikifuatiwa na Chipole na Spngea kujishindia tuzo ya mshindi wa tatu. Tuzo hizo zimetolewa kwa shule na siyo kwa wanafunzi.

5Washindi katika mdahalo kwa shule za sekondari mkoani Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (Jica) baada ya kukabidhiwa tuzo za IPad na ngao. IPad hizo zina notice za masomo yote kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita.

Leave A Reply