SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, leo ametembelea bandari ya Dar es Salaam na kujionea makontena yaliyotaka kusafirishwa nje ya nchi yakiwa na mchanga uliotoka katika migodi mbalimbali inayochimba dhahabu nchini.
Ndugai ameyaona makontena 256 yaliyokuwa njiani kusafirishwa kwenda nje ya nchi siku chache baada ya Rais Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo.
Baada ya ziara hiyo, Ndugai alisema aliambatana na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ili kupata ufafanuzi wa kina kutoka kwa viongozi wanaohusika na masuala ya madini kuhusu makontena hayo ili bunge kama chombo cha kushauri serikali lichukue hatua mara tu kikao cha Bunge la Bajeti kitakapoanza.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments are closed.