The House of Favourite Newspapers

Spika Mstaafu Anna Makinda Utapenda Alivyowanoa Madiwani Wanawake

0
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi akizungumza kwenye warsha hiyo kabla ya kumpisha Spika Mstaafu, Anna Makinda.

SPIKA mstaafu Anna Makinda, leo amewanoa madiwani wanawake wanaoendelea na warsha ya kuimarishwa kiuongozi inayoendele kwenye ofisi za Mtandao wa Jinsia (TGNP) zilizopo Mabibo Jijini Dar.

Spika Mstaafu Anna Makinda alivyoanza kutoa somo.

Wanawake hao wamedhamiria kuwa viongozi wa mfano kufikia kumiliki nafasi za uongozi kwa asilimia hamsini kwa hamsini na wanaume.

Akizungumza na madiwani hao, Spika Makinda aliwaasa kufanya mambo mbalimbali ili kuboresha nafasi zao hizo.

Baadhi ya mambo aliyowasisitiza ni pamoja na kushiriki shida na raha za wananchi, kushiriki miradi ya maendeleo na mambo mengine.

Diwani Monica (kushoto) na mwenzake wote kutoka Peramiho mkoani Ruvuma wakiimba nyimbo za hamasa wakati warsha hiyo ikiendelea.

Spika Makinda aliwataka madiwani hao kutojiweka nyuma kwa kujiona wao ni wanawake na kujipa majukumu madogo madogomadogo kama vile kupigia wageni kwenye matukio wanayotakiwa kushiriki moja kwa moja.

“Unakuta mkutano wa viongozi unaendelea eti, mheshimiwa diwani kwakuwa yeye ni mwanamke basi yuko jikoni na wamama wengine wanapika wanaume ndiyo wanasikiliza huku yeye akipitwa na yanayoendelea.

Spika Makinda akizidi kutoa somo kwa madiwani hao.

“Hapo ni lazima hoja za msingi wanazojadili wenzako zikupite, nawataka wanawake muamke.

“Siku hizi ulimwengu umeendelea kama ni shughuli za upishi kuna watu wanashughulika nazo kwa malipo hivyo ukiona katika tukio linalokuhusu kuna uhitaji wa kupikwa chakula toa maoni watafutwe wapishi ili huepukane na usumbufu huo na usikilize vizuri hoja zinavyoendelea”. Alisema Makinda.

Baadhi ya washiriki kutoka mkoa wa Ruvuma wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Baada ya kuwanoa vilivyo wanamama hao nao walielezea changamoto zao za kiungozi wanazokutana nazo kwenye maeneo yao ambapo nae kwa kutumia uzoefu aliwaelekeza jinsi ya kupambana nazo.

HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply