The House of Favourite Newspapers

Spika Ndugai Aagiza NIDA Waitwe na Kieleweke

0

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ameiagiza kamati ya mambo ya nje ya ulinzi na usalama ya Bunge hilo, kuwaita Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ili kuwahoji na kujua sababu inayokwamisha kasi ya utaoji wa vitambulisho vya Taifa kwa wananchi.

 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 2, 2021, Bungeni Dodoma, wakati wa mkutano wa tano, kikao cha kwanza cha Bunge la 12, baada ya kuibuka kwa mjadala ulioibuliwa na mbunge wa Makunduchi Ravia Faina, aliyehoji kwamba huenda fedha za wananchi zimeliwa licha ya NIDA kuongezewa mashine mbili lakini bado kasi ya uzalishaji na ugawaji wa vitambulisho hivyo ni ndogo.

 

“Kamati ya mambo ya nje ya ulinzi na usalama waiteni NIDA, hawafanyi kazi nzuri,, waiteni kieleweke, tumeanza nao kitambo sana ni kiswahili tu, kupitia kamati tutajua ni nini kinaendelea hapo NIDA ndiyo maana labda mbunge anahisi kuna hela zimeliwa,” ameagiza Spika Ndugai

Leave A Reply