The House of Favourite Newspapers

Spika Ndugai Aanika Kamati za Bunge

0

Spika wa Bunge, Job Ndugai juana Januari 18 amefanya utuezi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge 17. Taarifa iliyopatika tovuti ya Bunge imesema Spika amechukua hatua hiyo kwa mujibu wa ibara ya 96 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayolipa Bunge uhalali wa Kuunda kamati za Bunge za namna mbalimbali kadri itakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa madaraka yake.

 

Pia Katiba hiyo imeweka wazi kwamba Kanuni za Kudumu za Bunge zitafafanua muundo wa shughuli za Kamati za Bunge. Katika kamati hizo, kamati ya Kudumu ya Kanuni za Bunge inaongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika Dk Tulia Ackson na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi.

 

Wengine ni Abdullah Mwinyi, Ridhiwani Kikwete, Edward Olelekaita, Sebastian Kapufi, Jason Rweikiza, Dk Oscar Kikoyo, Simai Hassan Sadiki, Judith kapinga, Ramadhan Suleiman Ramadhan, Ally Mhata, Salome Makamba, Zaytun Swai, Jacob Priscus, Zainabu Katimba, Ng’wasi Kamani, Sylvia Sigula, Aida Khenani.

 

 

Nyingine ni Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Kamati ya masuala ya Ukwimu inayoongizwa, Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira inayoongozwa, Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kamati ya Utawala na Serikali za mitaa.

 

 

Nyingine ni Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, Kamati ya Miundombinu, kamati ya Nishati na Madini, kamati ya Bajeti, Kamati ya Sheria Ndogo, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).

 

 

“Mheshimiwa Spika amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Kanuni ya 135(3) na kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa katika kanuni ya 135(5). Baada ya uteuzi huo, Wajumbe wa kila Kamati wanawajibika kuchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 135 (10) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,” imesema sehemu ya taarifa ya Bunge.

Spika Ndugai Aanika Kamati za Bunge by Eddy Nevo

🔴#LIVE: DIAMOND ANAVUNJA UKIMYA, ANAZUNGUMZA NA WANAHABARI MUDA HUU…

Leave A Reply