The House of Favourite Newspapers

Spika Ndugai Azungumza na Waandishi wa Habari

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai anazungumza na waandishi wa habari jioni hii kuhusu mambo mbalimbali ambapo pia amesema wabunge wa viti maalum walioteuliwa na CUF ya Lipumba, wataapishwa kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu sakata la kashfa ya Lugumi na jeshi ola polisi, Ndugai ameeleza kwamba kamati ya bunge iliupitia mkataba wa kufunga vifaa vya kielektroniki kwenye vituo vya polisi nchini kuangalia kama kulikuwa na ufisadi kama ilivyobainishwa na mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali lakini bado kazi hiyo haijakamilika.

Kuhusu mgogoro unaoendelea ndani ya chama cha CUF, Ndugai amesema bunge kama mhimili, huwa unapokea taarifa kuhusu vyama kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa nchini na si vinginevyo kwa hiyo wanaheshimu na kuyafanyia kazi maelekezo kutoka kwa msajili na si kutoka kwa vyama moja kwa moja. Akasema Bunge haliwezi kuingilia mvurugano unaoendelea ndani ya chama hicho, kati ya pande mbili za Profesa Ibrahim Lipumba na maalim Seif Sharif Hamad, bali wao wenyewe ndiyo wenye jukumu la kumaliza tofauti zao.

 

Comments are closed.