The House of Favourite Newspapers

Spika wa Bunge la Marekani, Kevin McCarthy Ang’olewa Madarakani

0
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Marekani, Kevin McCarthy ameng’olewa madarakani.

Spika wa Bunge la Marekani, Kevin McCarthy ameng’olewa madarakani baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika tukio la kihistoria Jumanne ya Oktoba 3, 2023.

McCarthy amepigiwa jumla ya kura 210 kati ya kura 216 za kumtaka atoke madarakani, ambapo wabunge 8 wa chama chake cha Republicans waliungana na wabunge wa Democrats kumshinikiza atoke madarakani.

Afisa wa Bunge la Marekani, Steve Womack ameutangazia umma kuwa nafasi ya spika iko wazi baada ya spika kupigiwa kura za kumtoa madarakani.

Sababu kubwa ya spika huyo kuondoshwa madarakani, inaelezwa kuwa ni McCarthy kudaiwa kupitisha kwa siri kwa kushirikiana na Rais Joe Biden, muswada wa kuisaidia Ukraine, saa kadhaa chache kabla ya serikali kusitisha huduma zake.

Hii ni mara ya kwanza kwa spika wa Marekani kupigiwa kura ya kutokuwa na imani ambapo Patrick McHenry wa Nirth Carolina, anatajwa kukaimu nafasi hiyo mpaka uchaguzi wa spika utakapofanyika.

Leave A Reply