The House of Favourite Newspapers

Askari Polisi Ajipiga Risasi Kidevuni Mbele Ya Mpenzi Wake Na Kufariki – Video

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linapenda kutoa ufafanuzi wa tukio la kujiua kwa kujipiga risasi kwa aliyekuwa Askari J.2596 Konstebo wa Polisi Samwel Feston Kaziyote [24] wa kituo kikuu cha Polisi Mbeya.

Ni kwamba, Oktoba 02, 2023 majira ya saa 2:15 usiku huko maeneo ya Mtaa wa Mzumbe Forest ya zamani, Jijini Mbeya Askari huyo alijipiga risasi kidevuni na kusababisha kifo chake papo hapo.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokea baina yake na mpenzi wake baada ya marehemu kuacha lindo la Benki na kishakuondoka na silaha bunduki kwenda nyumbani kwa mpenzi wake huyo na kujipiga risasi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Leave A Reply