The House of Favourite Newspapers

Spika Wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda Atoa Neno Kuhusu Sensa Kwenye Warsha Na Wanahabari

0

Dar-es-Salaam 14 Machi 2024: Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda amesema kuwa wanasiasa wasifurahie tu matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, badala yake watambue kuwa inaweza kuwa mwiba kwao.

Makinda ambaye pia ni Kamisaa wa Sensa nchini ameyasema hayo wakati warsha ya siku mbili inayofanyika Machi 13-14, 2024 jijini Dar-es-Salaam ambayo imewakutanisha wanachama wa Chama Cha Waandishi wa Habari Dar Es salaam (DCPC) ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Katika warsha hiyo yametolewa mafunzo mbalimbali kuhusu sensa ikiwemo, takwimu za sensa ikiwa ni sehemu ya awamu ya tatu ya utekelezaji Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

“Tumewaambia wanasiasa wenzagu, sensa hii imefanikiwa lakini, kwenu ni kiboko, shangilieni lakini watu watakuwa wanauliza maswali kutokana na takwimu na maelezo yaliyomo kwenye matokeo ya sensa.

“Sisi tunafundisha mpaka chini kwa wananchi hivyo basi hilo kwa wanasiasa wakati ambapo taifa linatarajia kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu 2024 na Uchaguzi Mkuu mwakani 2025.

“NBS imeona umuhimu wa kuwapa mafunzo pia waandishi wa habari ili taaluma hiyo iwe ya kuaminika zaidi kwa takwimu.

“Waandishi wa habari mna nafasi kubwa katika suala hili na sisi tunawategemea. Tunategemea nchi yetu ifike mahali inazungumza habari za takwimu, sio tunazungumza maneno ya majungu majungu tu vitu vitu visivyoeleweka, hapana, tuzungumze maendeleo,” amesema Makinda.

Leave A Reply