The House of Favourite Newspapers

SportPesa Yashirikiana na Simba Kugawa Vifaa vya Michezo

0

Jumanne 18 Agosti, Dar es Salaam. Kampuni ya michezo na burudani SportPesa kwa kushirikiana na klabu ya Simba imegawa vifaa vya michezo kwa timu mbili jijini kuelekea maadhimisho ya Simba week 2020 chini ya udhamini wa SportPesa.

 

Akizungumza na waandishi wa habari viwanja vya Uhuru Meneja Uhusiano SportPesa Sabrina Msuya alisema “Leo tumegawa vifaa vya michezo kwa timu mbili ambazo zimependekezwa na uongozi mzima wa Simba wenyewe kuelekea kilele cha SportPesa wiki ya Simba”

“Lengo letu kuu kama wadhamini wakuu wa timu hii ni kukuza na kuendeleza michezo nchini hasa mpira wa miguu na ndio maana tumesaidia hizi timu zinazoshiriki ligi daraja la tatu ili kuweza kuwainua kwa namna moja ama nyingine”

 

“Tandale FC ma Dar City FC tumeanza nao msimu huu vile vile hili ni zoezi endelevu kwa mwaka jana tulikaribisha msimu mpya wa Simbakwa kusaidia timu tatu kutoka wilaya ya Kinondoni, Ilala pamoja na Temeke.

 

Kwa niaba ya klabu ya Simba Meneja Mashindano Hamisi Kissiwa aliongeza “Tunafuraha sana kuungana na SportPesa kwenye siku hii ya leo kuadhimisha na kusaidia timu hizi “

“SportPesa mnaweza mkaona huu ni msaada mdogo lakini kusema ukweli mnaenda kuwainua sana na kuwafanya wafikie ndoto yao”

 

Katibu mkuu wa timu ya Dar City FC Rajabu Samora alisema “Tunashukuru sana kampuni ya SportPesa kwa kutuona na kutambua mchango wetu kwenye mpira kwani tunapitia changamoto mbalimbali na hii leo wamedhihirisha kwa kutupatia vifaa vya michezo.”

 

Baadhi ya wachezaji wa timu hizi mbili walifanya mazoezi ili kuonyesha umati uwezo wao mara baada ya makabidhiano katika viwanja vya uhuru

Leave A Reply