The House of Favourite Newspapers

Benki ya NBC Yajikita Kukuza Michezo Vyuoni

0
Maofisa kutoka benki ya NBC wakitoa huduma za kibenki kwa washiriki wa bonanza hilo.

Benki ya NBC yaendelea kuchangia Maendeleo ya michezo katika vyuo nchini kwa kudhamini tamasha la michezo la “Daruso – DUCE day” katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam. Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka lilihusisha mchezo wa mpira wa miguu, mpira wa kikapu, netiboli, mpira wa wavu, Riadha na kuvuta Kamba.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)   wakishiriki mchezo wa netiboli katika bonanza la siku ya Daruso – DUCE.

Tamasha hilo la michezo lilikuwa mahususi kwa ajili ya kuwaaga viongozi wa Serikali ya Wanafunzi ambao wanamaliza muda wao na kukaribisha Uongozi mpya chuoni hapo. Benki ya NBC imetumia fursa ya michezo kukutanisha watu kutoka makundi mbalimbali ya kijamii.

Wafanyakazi wa benki ya NBC tawi la Chang’ombe wakiongozwa na Meneja wa tawi hilo, Bw. Aliko Mwamusako (wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya wanafunzi wa mwaka wa pili na wa kwanza, DUCE kwenye bonanza la siku ya Daruso.

Kivutio kikubwa kilikuwa ni mechi ya mpira wa miguu kati wanafunzi wa mwaka wa tatu dhidi ya timu ya mchanganyiko kwa wanafunzi wa mwaka wa pili na wa kwanza, ambao matokeo yalikuwa 1-1 hadi wa kawaida ulipokwisha, hivyo mchezo ulilazimika kuamuliwa kwa mikwaju ya penati.

Wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakishiriki mchezo wa kuvuta kamba kwenye bonanza la siku ya Daruso-DUCE.

Golikipa wa timu ya mwaka wa tatu ndiye alikuwa shujaa wa mchezo baada ya kupangua mikwaju miwili ya penati na kuipatia timu yake ushindi wa mabao 4-2.

 

Katika kusaidi Maendeleo ya Vijana, benki ya NBC inawalipia gharama za masomo Zaidi ya wanafunzi 30 ambao wana changamoto za kifedha chuoni hapo. Programu hiyo inawagharamia wanafunzi kutoka vyuo vitatu Zaidi, Chuo cha Udhibiti wa Fedha (IFM), Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE) na Chuo wa Wanyamapori MWEKA.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakishiriki mchezo wa mpira wa kikapu kwenye bonanza la siku ya Daruso-DUCE.

“Sisi kama NBC tawi la Chang’ombe tumedhamiria kuendeleza uhusiano mzuri tulionao na Chuo cha DUCE ili kuhakikisha tunawasaidia wanafunzi kadri tuwezavyo; na bonanza hili ni miongoni mwa jitihada zetu katika kuimarisha Umoja, afya njema na Elimu ya fedha. Lengo ni kuwaandaa vijana wanaohitimu wawe na uelewa wa kifedha.

 

 Ndio maana tumeanzisha “Malengo Account”, akaunti maalumu inayomuwezesha mteja kuhifadhi pesa zake na kuwa na uwezo wa kutoa mara moja tu kwa mwaka, huku ukiwekeza kiasi kidogo kuanzia Tsh 10,000 kupitia ATM zetu nchi nzima” alisema Aliko Mwamusako, Meneja wa NBC tawi la Chang’ombe.

Meneja wa Benki ya NBC tawi la Chang’ombe, Bw. Aliko Mwamusako akizungumza katika bonanza la Siku ya Daruso, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).

Pamoja na ajenda ya michezo, Benki ya NBC inatoa mafunzo juu ustadi wa ajira kupitia Programu ya ‘Wajibika’. Wajibika ni mkakati wa kuwafundisha vijana mbinu ambazo hawafundishwi sekondari wala Chuoni lakini ni muhimu katika kazi zao za baadae. Mbinu hizo ni pamoja na Ustadi wa kazi, stadi za fedha, Ujasiriamali na stadi za kuhusiana na watu. Kupitia Programu hii NBC imeshafundisha vijana Zaidi ya 9000 hapa nchini.

 

Baadhi ya wanafunzi hao waliipongeza benki hiyo kwa namna inavyoshirikiana na wanafuzi katika masuala mbambali yanayowahusu ikiwemo elimu na michezo huku wakitoa wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano huo.

Leave A Reply