The House of Favourite Newspapers

SportPesa Yazinduliwa Rasmi Hapa Nchini

0
Kampuni ya SportPesa yenye makao makuu yake nchini Kenya leo imezindua huduma zao nchini Tanzania.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiwa na viongozi wa juu wa SportPesa.
…Wakipiga makofi baada ya uzinduzi huo.
Wanahabari wakifuatilia uzinduzi huo wakiongozwa na Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally (wa kwanza kushoto mwenye sweta).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

 

Kiongozi wa SportPesa, akiongea jambo.
Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (kushoto) akiongea na Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo.
Wafanyakazi wa Global Publishers wakiongozwa na Saleh (wa pili kutoka kushoto), Nyange (kushoto) na Amani Madebe (kulia) wakiwa na Mr. SportPesa.
…Saleh Ally Jembe (kulia) akiwa na Edo Kumwembe, Msanii Fid Q na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu, Mwita.
…Saleh akimuonyesha jambo Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange Kaburu.
…Kaburu (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wanahabari.
…Saleh akiwa ma Mr. SportPesa.

Kampuni ya SportPesa yenye makao yake makuu nchini Kenya ambayo hivi karibuni ilikuwa ikitajwa kutaka kuzidhamini Simba na Yanga, leo imezinduliwa rasmi hapa nchini tayari kwa kuanza kazi zake za kuendesha michezo ya kubatisha (betting) lakini pia kuendeleza michezo mbalimbali ikiwemo soka.

Kuhusu kuzidhamini timu za Simba na Yanga uongozi wa kampuni hiyo umewataka wapenzi na mashabiki wa soka hapa nchi kuwa na subira kwani Jumamosi hii kila kitu kitawekwa hadharani.

Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba ambaye pia amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga alisema kuwa kuanzia Jumamosi hii itajulikana na timu zipi ambazo watafanya nazo kazi hapa nchini.

Hafla hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali maarufu hapa nchini akiwemo pia Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.

Kwa habari zaidi tembelea Global TV Online inayopatikana kwenye mtandao wa Youtube.

(PICHA: GLOBAL TV ONLINE)

Leave A Reply