The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaipiga Kagera Sugar bao 2-1 Uwanja wa Taifa

0
Kikosi cha Yanga kilichoanda dhidi ya Kagera Sugar leo.

Mchezo umemalizika DK 90 Yanga wanaondoka kifua mbele…

Dk 3 zimeongezwa kabla mchezo kumalizika

Dk 87, Mbaraka Yusuf wa kagera Sugar anapewa KADI NYEKUNDU

Dk 85 Yondani ameumia na anapewa matibabu
Dk 82, Fakhi analala na kuokoa mbele ya Msuva na kuwa kona, inachongwa lakini haina msaada
SUB Dk 78 Chirwa anakwenda benchi upande wa Yanga na nafasi yake inachukuliwa na Matheo Anthony
Dk 76 kwa mara nyingine, Kaseja anaonyesha umahiri wa juu kabisa baada ya kuruka na kudaka vizuri kabisa hapa kichwa kilichopigwa vizuri kabisa hapa na Tambwe

Dk 78 Yanga wanafanya mabadiliko, Chirwa anatolewa kwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Matheo Anthony

Dk 76 kwa mara nyingine, Kaseja anaonyesha umahiri wa juu kabisa baada ya kuruka na kudaka vizuri kabisa hapa kichwa kilichopigwa vizuri kabisa hapa na Tambwe

Dk 74 Mbaraka Yusuf anaangushwa na Kagera wanapiga faulo lakini haileti madhara

Dk 72 Tambwe anaruka na kupiga kichwa kizuri

Dk 61, Fakhi na Kaseja walijichanganya hapa na mpira unatoka na kuwa kona
SUB Dk 58 Kagera wanamtoa Babu Seif na nafasi yake inachukuliwa Anthony Matoghola

Goooooooooooal Dakika ya 47 Chirwa anaiandikia Yanga bao la Pili.

Msuva akishangilia baada ya kutupia bao la kwanza.

-GOOOOOOOOOOOO Mbaraka Yusuf anaachia mkwaju mkali kabisa na kuandika bao safi kwa Kagera
DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 45, Yondani analala na kuokoa mpira hapa dhidi ya Ame Ali
Dk 43 Kakolanya anafanya kazi ya ziada kuokoa mkwaju mkali wa Mbaraka Yusuf na kuwa kona. Inachongwa hapa lakini haina manufaa
Dk 41 Mwinyi Haji anamuangusha Mangoma ambaye alijaribu kumtoka hapa

Dk 43 Kakolanya anafanya kazi ya ziada kuokoa mkwaju mkali wa Mbaraka Yusuf na kuwa kona. Inachongwa hapa lakini haina manufaa
Dk 41 Mwinyi Haji anamuangusha Mangoma ambaye alijaribu kumtoka hapa


GOOOOOOOOOOOO Dk 39 Msuva anaruka na kupiga kichwa safi akiunganisha kona ya Mwashiuya na kuiandikia Yanga bao safi kabisa
Dk 35, Mangoma nje ya 18, anaachia mkwaju mkali hapa, hata hivyo hakulenga lango

Dk 31, Fakhi anautoa mpira nje tena na kuwa kona. Inachongwa vizuri hapa, Mwashiuya anajaribu kufanya yake lakini anakosea
Dk 30 Kessy anaachia mkwaju mkali kabisa lakini hakuwa amelenga lango
Dk 26 sasa, Yanga wanaonekana kujipanga vizuri kupeleka mashambulizi mengi lakini Kagera Sugar wanaonekana wakiwatuliza Yanga
Dk 22, Yanga wanapata koa nyingine baada ngoma kupiga fyongo. kona inapigwa lakini Kagera wameokoa

Kikosi cha Kagera Sugar.

Dk 16, Fakhi anafanya kazi ya ziada, analala na kuokoa mpira dhidi ya Chirwa na kuwa kona. Inachongwa vizuri lakini Yanga wanaokoa
Dk 14, Mbaraka Yusuf anamporonyoka Cannavaro ambaye analazimika kumkinga na kumuangusha. Cannavaro ameonyesha uzoefu wake maana ilikuwa ni hatari

Dk 13, krosi safi ya Kessy, Msuva anaachia bunduki kali, lakini hakulenga lango. ilikuwa hatari hapa
Dk 10 sasa, Kaseja yuko chini pale akitibiwa. Inaonekana alipata maumivu wakati akijaribu kuokoa
Dk 10, Yanga wanafanya shambulizi jingine kali kabisa hapa, lakini Kaseja anaruka kama nyani na kuokoa, lakini amegongwa na kuanguka chini
Dk 6, krosi safi ya Kessy hapa lakini Fakhi anaruka vizuri na kuokoa hapa
Dk 4, krosi nzuri ya Niyonzima anajaribu hapa Chirwa lakini inashindikana
Dk 1, Yanga imeanza kwa kasi ikiwa imepania kufunga bao la mapema

(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)

Leave A Reply