The House of Favourite Newspapers

Spoti Hausi LIVE: Haruna Niyonzima Afunguka Alivyotoka Yanga Kwenda

0

 

BAADA ya minong’ono mingi juu ya kiwango chake kushuka, kiungo mchezeshaji mpya wa Simba Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amevunja ukimya na kufunguka huku akiahidi kurejesha kukirejesha kabla ya mechi dhidi ya Yanga.

Hiyo, ikiwa timu hiyo tayari imecheza michezo yake minne ya Ligi Kuu Bara huku akikosa mchezo mmoja pekee dhidi ya Mwadui FC uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru kutokana na kuugua homa.

Mnyarwanda huyo, alijiunga na Simba kwenye msimu huu wa ligi kuu akiwa kama mchezaji huru baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumalizika mwisho mwa msimu uliopita.

Akizungumza Niyonzima amezisikia lawama nyingi za wazi kutoka kwa viongozi na mashabiki wa Simba wakimtuhumu kuwa kiwango chake kimeshuka kitu ambacho siyo sahihi.

Niyonzima alisema, ukweli ni kwamba alikosa maandalizi mazuri ya ‘Pre Seasson’ pamoja na wenzake kutokana na kubanwa na baadhi ya majukumu akiwa nyumbani kwao Rwanda huku timu ikiwa kambini nchini Afrika Kusini ikijiandaa na ligi kuu.

Alisema kuwa, kikubwa kiwango chake haikijashuka kama inavyoelezwa, yeye tatizo lake lipo kwenye fitinesi ambayo alichelewa kuitengeneza kwenye pre seasson pamoja na wenzake.

Mnyarwanda huyo alisema, amepanga kukutana na Kocha Mkuu wa timu hiyo kwa ajili ya kuzungumza naye na kikubwa ataomba aandae au apewe programu maalumu ya mazoezi ya kuongeza fitinesi kwa maana na asubuhi kwenye gym na jioni kwenda kukimbia ufukweni.

“Minong’ono na maneno mengine makali ya wazi yote nimeyasikia kutoka kwa wanachama na baadhi ya viongozi wa Simba kuhusiana na mimi kiwango changu kimeshuka, kiukweli maneno hayo yananiumiza na kunikosesha amani.

“Hivyo, basi nimeshindwa kuendelea kukaa kimya na kuamua kuweka wazi kila kitu juu ya taarifa yangu, niseme tu kiwango changu hakijashuka tatizo pre seasson yangu haikuwa nzuri tofauti na wenzangu waliokwenda kambini Afrika Kusini mimi nikiwa nyumbani nikimaliza matatizo.

“Na kipindi hicho Simba imeweka kambi yake Sauzi, mimi sikuwa na timu yoyote kwani mkataba wangu ulikuwa ummalizika Yanga, hivyo nilikuwa nimepumzika kwa muda wa mwezi mzima kabla ya kurejea siku moja kabla ya mechi na Rayon SC ya Rwanda kwenye sherehe ya Simba, hivyo nilicheza nikiwa sijafanya mazoezi.

“Hivyo, leo (jana) ninatarajia kukutana na kocha wangu Omog kwa ajili ya kumuomba anipe au niitengeneze programu yangu mazoezi ya fitinesi ya gym na ufukweni kwa muda wa wiki mbili pekee ili niwe fiti kabla ya mechi na Yanga.

“Niwaombe radhi mashabiki wa Simba, ninajua wanataka kuniona Niyonzima yule aliyekuwa anaichezea Yanga, ninaomba muda wakijiweka sawa ninawahakikishia watafurahi tu, wanafahamu jinsi usajili wangu ulivyokuwa na presha kubwa”alisema Niyonzima.

 

Leave A Reply