The House of Favourite Newspapers

SPOTI HAUSI: Yachambua, Uchaguzi TFF, Ligi ya Vodacom na Usajili

0
Kutoka kushoto ni Wilbert Molandi, Philip Nkini, Aaron Nyanda na Elius Kambili.

 

SPOTI HAUSI leo ikiwa na mgeni aliyewahi kuwa mchezaji wa Yanga, Aaron Nyanda, imechambua kwa ‘marefu’ uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) unaotegemewa kufanyika mwishoni mwa wiki hii, Agosti 12 mjini Dodoma ili kupata uongozi ambao utasimamia shughuli zote za soka kitaifa.

 

Kabla ya uchambuzi, Nyanda ambaye anagombea nafasi ya ujumbe katika TFF alitumia fursa hiyo kujieleza kwa kirefu kuhusu nia, dhamira na malengo yake katika kuwania nafasi hiyo.

 

Uchambuzi uliofanywa na timu ya Spoti Hausi ikijumuisha wachambuzi wa ‘ndani ya nyumba’ ambao ni Elius Kambili, Philip Nkini, Wilbert Molandi na mgeni maalum, Aaron Nyanda, ulijikita katika masuala ya usajili wa timu za Ligi Kuu nchini inayojulikana kama Ligi ya Vodacom na kufanya tathmini ya utabiri wa jinsi timu zitakavyokuwa na nguvu mpya katika msimu huu.

 

Ligi Kuu ya England pia inayotegemewa kuanza wikiendi hii, ilipewa nadhari kubwa kwani ni moja ya ligi zinazofuatiwa kwa ukaribu na wapenzi wa soka nchini.

 

Leave A Reply