The House of Favourite Newspapers

Polisi Yaua 13 Ikidai ni Wahalifu Kibiti

0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Siro (katikati aliyeshika kiuno)  akiongea na viongozi wa jeshi lake Tangibovu, Kibiti, wakati wa kuonyesha silaha walizokamata kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa wahalifu.

JESHI la Polisi nchini Tanzania limesema wahalifu 13 wameuawa katika majibizano ya risasi katika eneo la Tangibovu lililopo katika kijiji cha Miwaleni, tarafa ya Kibiti mkoani Pwani na kukamata bunduki nane, pikipiki mbili na begi la nguo.

Jeshi hilo limeendeleza jitihada zake kuhakikisha mkoa wa Pwani na maeneo yake ya jirani yanakuwa salama na yenye amani kwa kuendelea kupambambana na wahalifu mbalimbali waliojificha mkoani humo  ambao wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya kihalifu.

…Akiongea (kulia) na wananchi wa Kibiti.

Rais John Pombe Magufuli alipokuwa katika ziara mkoa wa Pwani mwezi Juni mwaka huu aliwataka wahalifu wote waliopo mkoani humo waache mara moja kufanya matukio ya kihalifu, ambapo  pia Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro aliwataka wahalifu kuacha mara moja uhalifu mkoani humo na kuwaambia kuwa mkono wa dola utawafikia kama wataendelea.

 

Mkoani Pwani zaidi wa watu 30 wameuawa na watu wasiojulikana kwa vipindi tofauti  huku jeshi la polisi nalo likifanikisha kuwaua zaidi ya wahalifu 20 wanaodaiwa kuhusika na matukio mbalimbali yakiwemo yaliyokuwa yakifanyika mkoani humo na maeneo jirani.

Polisi Waua Majambazi Wanne KIBITI Wanaodhaniwa Kujihusisha na Mauaji Pwani

Leave A Reply