The House of Favourite Newspapers

SPOTI XTRA SASA HALISHIKIKI MITAANI – PICHAZ

HAKIKA ilikuwa ni Jumapili nyingine ya maajabu kabisa mitaani, pale gazeti bora kabisa la michezo kwa sasa nchini Tanzania, Spoti Xtra, lilipoendelea kuwapa wasomaji wake habari mbalimbali za michezo, burudani, makala na hadithi za kusisimua kutoka kwa waandishi mahususi kabisa wa michezo wa gazeti hili.

Timu ya masoko na usambazaji ya Global Publishers Ltd ilifanya promosheni kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam sehemu za Kisukuru, Tabata-Bima, Kimenya, Kimanga, Tabata Camp, na sehemu nyingine.

 

Maofisa masoko wa wakifunga nailoni kwenye meza ya muuza magazeti, Hassani Juma maeneo ya Tabata – Kimanga.

 

Timu hiyo ya mauzo ilishuhudia wasomaji mbalimbali wakiligombania gazeti  la Spoti Xtra kama njugu, huku wengi wakijipatia fursa kabambe za zawadi mbalimbali za jezi origino za timu wanazozishabikia kupitia gazeti hili pendwa kabisa.

Pia wameshauri gazeti liendelee kusambazwa zaidi maana limekuwa ni gazeti tofauti kwa maana lina habari za uhakika na za kusisimua. Vilevile timu ya masoko iligawa vifuniko vya plastiki (nailoni) kwa ajili ya kufunikia  magazeti nyakati za muv kwa baadhi ya mavenda kama inavyoonekana kwenye picha.

 

Na Mussa Mgema

Daktari Amchoma Mtoto Sindano ya SUMU, Mkono Wakauka!

Comments are closed.