The House of Favourite Newspapers

St Mary Goreti Yaonesha Mfano Wa Kuigwa

0
Wadau mbalimbali wakichangia damu katika zoezi la upimaji afya na kuchangia damu katika Shule ya St Mary Goreti iliyopo Moshi.

MBUNGE wa Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro Bw Priscus Tarimo, ameupongeza uongozi wa shule ya sekondari ya St Maria Goreti mchangao mkubwa inayotoa katika kukuza sekta ya elimu na mchango wa shule hiyo kwa jamii kwa ujumla

Bw Tarimo alitoa pongezi hizo wakati wa kambi maalum ya kupima afya na kuchangia damu iliyoandaliwa na uongozi wa shule hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yanayooendelea ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya St Mary Goreti Sr Clementina Kachweka akizungumza wakati wa zoezi la upimaji afya na kuchangia damu katika viwanja vya shule hiyo.

“Shule hii ilianza kama shule ya sekondari ya kawaida, baadaye ikawa ya hadi kidato cha sita; sasa hivi uongzi wa shule hii umeanzisha shule ya awali pamoja nay a msingi, haya ni mafanikio makubwa kwa shule yenu na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya elimu hapa nchini”, alisema.

Aidha aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuchangia maboresho ya mazingira mkoani Kilimanjaro kwa kuchangia miche ya miti na uandaji wa miti katiak wilaya zote za Mkoa kama sehemu ya maadhimisho.

Wanafunzi wa shule ya St Mary Goreti wkaifuatilia matukio ya zoezi la upimaji afya na kuchangia damu katika viwanja vya shule hiyo.

“Nimeelezwa ya kuwa mmechangia miti 2,000 itakayopandwa maeneo mbalimbali hapa mkoani Kilimanjaro, huu ni mchango mkubwa katika kuboresha mazingira haswa ikitiliwa maanani ya kuwa moja wapo ya ajenda za serikali ni kuhakikisha mazingira yanaboreshwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi”, alisema.

Kuhusu kambi hiyo, Bw Tarimo alisema pia ni njia nzuri kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 25 ya shule ambapo alisema wananchi watapata fursa ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wananchi wengine sambamba na kupima hali zao za afya bure.

Bw Tarimo ambaye katika hafla hiyo alijisajili kama mshiriki wa mbio zilizoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho hayo, pia alioupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuandaa mbio hizo ambazo alisema zitachangia kuboresha maisha ya washiriki sambamba na kukuza sekta ya michezo.

Awali akimkaribisha Mbunge huyo kutoa salamu zake, Mkuu wa shule ya sekondari ya St Maria Goreti Sr Clementina Kachweka, alisema kambi hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuchangia damu kwa wahitaji, haswa ikitiliwa maanani mahitaji ya damu yamekuwa ni makubwa katika taasisi za tiba mkoani Kilimanjaro.

“Mbali na kuchangia damu, pia watu watapata fursa za kupima afya zao bure, lengo ni kuwapa watu kuweza kujua hali zao za kiafya na pale anapogundulika kuwa na maradhi aweze kuanza tiba mapema”, alisema.

Aliishukuru hospitali ya KCMC ya Moshi kwa kuwa mstari wa mbele katika kuratibu zoezi hilo la upimaji afya na kuchangia damu huku wakisaidiwa na wataalamu wengine kutoka Hospitali ya St Joseph, Hospitali ya Huruma na Masispaa ya Moshi (kitengo cha Damu Salama). Zaidi ya watu 1000 wakiwemo wanafunzi walipima afya na kupata ushauri mbalimbali na watu 50 walichangia damu itakayookoa maisha ya watu 150.

Sr Clementina aliendelea kusema kuwa mbali na zoezi hilo, pia tayari uongozi wa shule hiyo umeshafanya matukio mengine ikiwemo uzinduzi wa maadhimisho hayo ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo na ugawaji wa miti 2,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambayo itapandwa maeneo mbalimbali mkoani humo.

“Mbali na shughuli hizo, pia zitafuata shughuli zingine ambazo ni pamoja na mbio/matembezi ya hisani km 10 na km 5 zitakayofanyika Agosti 26, 2023 na ambazo usajili wake umeanza leo, (July 7)”, alisema.

Shughuli zote za kuelekea Jubilee ya miaka 25 ya St Mary Goreti zinaratibiwa na kampuni ya Executive Solutions Ltd, Moja makampuni yanayoongoza nchibi katika kuratibu matukio na masuala ya habari.

Leave A Reply