The House of Favourite Newspapers

Staa wa Singeli… ni zamu ya Kinondoni, Ilala

0

sholo mwambaBAADA ya kuzind-uliwa rasmi Agosti 20 na 21 pande za Zakhem-Mbagala jijini Dar, lile shindano la kusaka staa wa kuimba Singeli kwa Jiji la Dar linaendelea na sasa litatua Wilaya ya Kinondoni katika Viwanja vya Mwinjuma, Mwananyamala na Wilaya ya Ilala katika Viwanja vya Buguruni-Ghana.

Akizungumza na Showbiz, mratibu wa shindano hilo lililojizolea umaarufu, Juma Mbizo alisema kuwa katika kila wilaya wanatarajia kupata washindi 12 na baada ya hapo watamalizia Wilaya ya Temeke na Kigamboni kisha watafanya mchujo wa kuelekea nusu fainali.

“Katika kuelekea fainali kila wilaya itatoa washindi watatu ambapo tutahitimisha rasmi Septemba 10, mwaka huu pale Dar Live-Mbagala, Zakhem jijini Dar na kumpata staa wa kuimba nyimbo za Singeli,” alisema Mbizo.

Leave A Reply