The House of Favourite Newspapers

Stamina, Jay Moe, Young Killer, Wafunika Mkesha wa Mwaka Mpya Dar Live

Jay Moe akikamua.

WAKALI wa HipHop Bongo, Stamina, Jay Moe na Young Killer jana walifunika katika Show ya Kibabe iliyofanyika kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya 2018 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

Young Killer akikinukisha.

Show hiyo ilianza kwa kutoa nafasi kwa wasanii chipukizi kisha Msanii Papaa Masai akapanda jukwaani na kutoa burudani ya nguvu iliyowashangaza mashabiki wengi kwa uwezo wake wa kutawala jukwaa.

 

Killer akifanya yake kwenye jukwaa la Dar Live.

Stamina, Killer na Jay Moe kama kawaida yao kwa nyakati tofauti kila mmoja alipoingia stejini mlipuko wa kelele za shangwe ulisikika kutoka kwa mashabiki zao huku shoo ikinoga na kuonyeshana umwamba wa nani mkali kati yao.

Alicho kifanya Young Killer kwenye stage Dar live Usiku wa Show za Kibabe

 

Mashabiki nao bila kubaki nyuma walikuwa waki-enjoy ngoma zilizokuwa zikiporomoshwa na Ma-DJ na shoo kutoka kwa Marapa hao. Hakika ilikuwa ni shoo ya kihistoria.

Mashabiki wakishangweka.

Kati ya Marapa hao, Jay Moe alitangulia na kufanya makamuzi ya nguvu baadaye Young Killer aliyekimbiza mchakamchaka na time ilipowadia akapanda Stamina mwenyewe aliyeziamsha Shangwe za Mwaka Mpya 2018.

Killer na mashabiki, palikuwa hapatoshi.

 

Stamina akikamua.

 

Shoo likibamba.

 

Shoo ikibamba.

 

Stamina kiboko.

 

NA ISSA MNALY NA GABRIEL NG’OSHA

Comments are closed.