The House of Favourite Newspapers

Mashine 3 Za CAF Mlangoni Yanga Kuibomoa Klabu ya Asec Mimomas

0
Zoungrama Mohammed

YANGA kwa sasa wanachokifanya ni kutaka kuibomoa Klabu ya Asec Mimomas hiyo ni baada ya kuhusishwa na usajili wa wachezaji watatu kutoka katika timu hiyo ambao wote wamefanya vizuri msimu uliopita.

Asec ambao wanashiriki ligi kuu ya nchini Ivory Coast, kwa msimu uliopita walifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo huku kwenye michuano ya kimataifa wakifika hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Chanzo chetu cha ndani kutoka nchini Ivory Coast tayari kimeliambia Championi Ijumaa kuwa, Yanga wapo katika mipango ya kuibomoa timu hiyo huku wakihusishwa na usajili wa wachezaji watatu ambao ni beki wa kulia Yao Attohoula, kiungo wa kati Zoungrama Mohammed na winga Kramo Kouame Aubin.

Kramo Kouame Aubin

“Ni kweli Yanga wapo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji kutoka ndani ya ASEC Mimosas, kuna wachezaji watatu ambao Yanga wapo katika mipango ya kuwasajili na sio lazima wawasili wote lakini kati ya hao kuna ambao watawasajili.

“Yupo namba sita Zaongram, beki wa kulia Yao na winga Aubin Kramo, hawa wote wapo katika mipango ya Yanga japo siwezi kufahamu kama wote watasajiliwa lakini kikubwa ni kwamba wote mikataba yao na Asec Mimosas imemalizika jambo ambalo ni rahisi Yanga kuwapata,” kilisema chanzo cha kuaminika.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe simu yake haikuwa hewani.

Na Marco Mzumbe

#EXCLUSIVE: SHAMSA FORD AMEJIBU -“MTOTO WA MUME WANGU ni WANGU, MIMI NDIYE MRS. HUSSEIN, IMESHAKUA”

Leave A Reply