Stan Bakora ‘ajimilikisha’ video Queen

tunda vs stanKomedian matata Bongo, Stanley Yusuph ‘Stan Bakora’ akiwa na  video Queen Tunda.

Musa mateja
KOMEDIAN matata Bongo, Stanley Yusuph ‘Stan Bakora’, amenaswa akijimilikisha Video Queen mmoja aitwaye Tunda na kujikuta akileta gumzo kubwa kwa wakazi wa Jiji la Arusha waliowashuhudia wawili hao wakijiachia kwa raha zao.

Chanzo chetu makini kilivujisha ubuyu kuwa ishu hiyo ya aina yake ilitokea juzikati jijini humo ambapo wawili hao walikwenda kwa ajili ya shoo iliyokuwa ikitumbuizwa na Mbongo Fleva, Diamond Platnumz huku Stan na Tunda wakisindikiza makamuzi hayo.

Wawili hao walionekana mitaani wakiwa wamegandana kitu ambacho kiligeuka kivutio kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu waliowashuhudia kuamini wazi kuwa wanatoka kimapenzi.

STANAlipovutiwa waya Stan ili kujua kama amejimilikisha jumla mrembo huyo, alijibu:
“Kweli kaka nipo na Tunda na tunafanya yetu si unajua huyu ni mtu wangu sana, lazima watu wasiojua lolote juu yangu na Tunda wakituona ilikuwa ni rahisi kusema lolote maana nikiwa naye huwa najiachia ninavyoweza hata yeye hivyohivyo maana tumezoeana kinoma,” alisema Stan.


Loading...

Toa comment