The House of Favourite Newspapers

Ufahamu ugonjwa wa endometriosis unaowasumbua wanawake-3

0

SOC 152C endometriosis picKaribu msomaji katika ukurasa huu ambao umekuwa ukikupa maarifa muhimu ya afya zetu. Leo tutaendelea na tatizo la Endometriosis. Wiki iliyopita tuliangalia dalili za ugonjwa huu na jinsi ya kupunguza homoni au kuweka uwiano mzuri wa homoni ili kuondokana na tatizo hili. Leo tutaangalia njia zinazotumika kubaini tatizo hili mwilini na kupata ushauri wa kutunufaisha. Fuatilia makala haya utapata maarifa muhimu juu ya tatizo hili la Endometriosis.

Endapo mwanamke atapata dalili za ugonjwa huu ni vyema akawasiliana na kumwona daktari kwa ajili ya uchunguzi.

Vipimo vya picha, vipimo hivi ni kama Ultrasound pamoja na MRI (Magnetic Imaging Resonance). Vipimo hivi ni vile ambavyo hupiga picha ndani ya mwili ili kuona kama kuna uvimbe au tatizo lolote lile linaloweza kuonekana katika picha.

Laparascopy, kipimo hiki kinahusisha upasuaji na daktari kuweza kuingiza kipimo hiki ndani ya mwili kuweza kuona kama kuna uvimbe.

Hii huwa ndiyo njia ya kuhakiki na kujiridhisha kama kweli mgonjwa ana ugonjwa wa Endometriosis. Sababu ni kuwa njia hii huwezesha wataalam kuchukua sehemu ndogo ya tishu ya uvimbe kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa kimaabara.

Uchunguzi wa nyonga kuona kama kuna aina yoyote ya uvimbe au uvimbe katika kizazi. Wakati mwingine uvimbe ulio mdogo huwa ni ngumu kugundulika.

Dawa za maumivu na uvimbe
hutumika kutibu Endometriosis, Paracetamol zaweza kutumika wakati wa hedhi kama dalili za ugonjwa hazipo kwa kiasi kikubwa.

Dawa za maumivu zenye kuondoa uvimbe (anti inflammatory) pia zaweza kutumika, dawa hizi ni kama Naproxen, Ibuprofen na Aceclofenac. Mwanamke anaweza kutumia dawa hizi kama hazitamletea madhara. Dawa hizi ni zaidi ya Paracetamol kwa kuwa zinatibu uvimbe na maumivu ukilinganisha na Paracetamol ambayo hutibu maumivu pekee.

Dawa zenye mchanganyiko na kodeini, mfano Codeine na Paracetamol, zinakuwa na uwezo wa kutuliza maumivu makali. Hizi zaweza kutumika kama dawa za maumivu na uvimbe hazitasaidia. Dawa zenye kodeini zaweza kusabisha mgonjwa kukosa choo (constipation) .

Ikumbukwe kuwa Ostrogeni ni homoni ambayo hutengenezwa katika ovari (ogani ambayo hutengeneza mayai ya uzazi). Seli ambazo hujenga ukuta wa ndani ya uzazi kila mwezi, zinahitaji homoni ya Ostrogeni kuishi na kukua.

Seli hizi ambazo hukua nje ya tumbo la uzazi na kusababisha ugonjwa pia huhitaji homoni hii ya Ostrogeni.

Tiba ya homoni hufanya kazi kwa kupunguza kiasi cha Ostrogeni kinachotengenezwa mwilini na hii huathiri seli zinazojenga ukuta wa uzazi nje ya kizazi kushindwa kuendelea kuishi na kukua. Kwa kutumia tiba hii seli hizi husinyaa na hata kutoweka kabisa .

Upasuaji hufanyika kuondoa uvimbe na hii huongeza na kuboresha nafasi ya mwanamama kupata ujauzito kama ugumba ulisababishwa na Endometriosis.

Kwa wanandoa waliomaliza kupata watoto na matibabu mengine yameshindikana, upasuaji wa kuondoa kizazi (hysterectomy) hufanyika. Pia uchaguzi wa kuondoa Ovari huweza kufanyika, kwa kuwa Ovari hutengeneza homoni ya Ostrogeni, hii itasababisha dalili za ugonjwa huu kuondoka.

Lakini pamoja na tiba hizo kuwasaidia watu wengi, Sigwa Herbal Clinic tuna mimea tiba yenye uwezo wa kuyeyusha vimbe bila kufanya upasuaji, pia tuna mimea tiba ambayo inaweka uwiano mzuri wa homoni mwilini.

Nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume unaweza ukawatembelea katika vituo vyao vilivyopo nchi nzima kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu.

Leave A Reply