The House of Favourite Newspapers

Stanbic Yaungana na Wadau Kutoa Mafunzo kwa Wajasiriamali wa Arusha

0
Mkuu wa Huduma za kibenki wa benki ya Stanbic, David Robogo (Wapili kulia) akizungumza katika warsha maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na wa kati iliyoandaliwa na benki hiyo hivi karibuni kama sehemu ya uzinduzi wa suluhisho maalum la wateja hao jijini Arusha hapo jana. Pia kwenye picha ni Mwakilishi kutoka TRA Bi. Enni Andrea Mwanga (Kulia), Mwakilishi wa Manispaa ya Arusha, Privanus Katinhila (Katikati), Mwakilishi wa wateja , Grace Lyatuu (Kushoto) na John Mosha Mkuu kitengo cha Vehicle and Asset Financing VAF (Wapili kushoto).

 

 

Arusha, 13 Oktoba 2022: Takribani wanyabiashara 120 jijini Arusha wamehudhuria warsha ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya Stanbic chini ya kitengo cha Stanbic Incubator (Uatamizi), kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka TRA, SIDO na Manispaa, kutoa mafunzo kuhusu Nafasi ya Ubunifu na Teknolojia katika kuendesha na kukuza Biashara na Sheria, Kanuni na Taratibu za Biashara za kila siku.

 

Semina hii ni muendelezo wa shughuli za uzinduzi wa huduma ya Mpambanaji ambayo ilizinduliwa rasmi hivi karibuni jijini Mwanza. Kwa upekee kabisa benki hiyo imewaletea huduma ya Mpambanaji wakazi wa Arusha kupitia warsha ya mafunzo ambayo lengo lake kuu ni kuhakikisha wajasiriamali wanafahamu nyenzo muhimu za kukuza biasharazao.

 

Akizungumza katika warsha hiyo Charles Mishetto, Mkuu wa kitengo cha Biashara ndogo na za kati wa benki hiyo alisistiza dhamira ya benki katika kuchangia ukuaji wa sekta ya biashara ndogo na kati nchini na si tu kwa huduma za kifedha bali pia kwa kuwawezesha kuboresha biashara zao na kuwaongezea upatikanaji wa masoko ili waweze kufikia malengo yao.

 

Naye Mkuu Kitengo, Stanbic Biashara Incubator (uatamaizi) Kai Mollel alisema;

“Kitengo cha Stanbic Biashara Incubator kina malengo ya kutoa mafunzo, kuunganisha masoko, na kuwaunganisha na mitaji wafanyabiashara wadogo na kati.

 

Huduma hizi za kuchechemua, kulea na kuatamiza biashara zina akisi ahadi ya benki ya kuwezesha wafanyabiashara ili kukuza uchumi wa nchi. Hadi sasa wamefikiwa wafanyabiashara 250 Kutoka sekta mbalimbali mikoa ya Mwanza, Dar es salaam na Arusha.”

 

Kitengo hicho ni sehemu ya huduma zinazotolewa kwa wapambanaji. “Kupitia suluhisho la Mpambanaji, tunataka kuhakikisha wajasiriamali wanafikia malengo yao na wanajenga uwezo wa kushindana katika masoko ya kimataifa” Mollel, aliongeza.

 

Mmoja wa washirika wa warsha hiyo, Pendael Simion alisema warsha hiyo imemwezesha kuona upana wa huduma zinazotolewa na benki hiyo kuanzia kwa mfanyabiashara mmojammoja hadi kwa vikundi, na kilichomfurahisha zaidi ni kuwa benki hiyo imeonesha kuwajali wateja wao kwani kwa mafunzo wanayotoa yanasaidia kuhakiksha wafanyabiashara wanakua na biashara endelevu.

 

Huduma ya Mpambanaji inajumuisha huduma mbalimbali, ambazo ni; Akaunti mahususi kwa wajasiriamali (akaunti ya Mpambanaji, Vikundi, na Saccos), programu ya incubator (programu inayozingatia kujenga uwezo), Huduma za kibenki bila mipaka, mikopo ya vyombo vya usafiri, huduma za Bima, Huduma ya kufanyabiashara kati ya Tanzania na China, pamoja na huduma mpya ya Wakala wa Benki – Stanbic Wakala –yenye zaidi ya mawakala 500 wanaoongeza uwepo wa huduma za benki hii nchini.

Leave A Reply