The House of Favourite Newspapers

Stars Yapanda Kwa Nafasi Nne Tu Fifa

Taifa Stars (2)

Kikosi cha Taifa Stars.

TANZANIA kupitia Taifa Stars imefanikiwa kupanda kwa nafasi nne kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na sasa ni ya 156 kwa mujibu wa orodha iliyotoka juzi.

taifa-stars_1.jpg

Stars inayonolewa na Kocha Charles Boniface Mkwasa, imekuwa na kipindi cha kupanda na kushuka kwenye viwango hivyo vya Fifa ambapo Januari mwaka huu ilikuwa ya 126 na Februari ikapanda kwa nafasi moja kabla ya Aprili kushuka na kuwa ya 130 na baada ya hapo ikawa inazidi kupumulia mashine.

Mara ya mwisho yaani mwezi uliopita ilikuwa nafasi ya 160 kabla ya juzi kupanda kwa nafasi nne na kuwa ya 156. Kwa dunia Argentina inaongoza ikifuatiwa na Brazil.

halotel-strip-1-1

Comments are closed.