The House of Favourite Newspapers

Stendi Mwenge Kuanza Kutumika Machi Mwakani

0

 

KITUO cha mabasi cha Mwenge kitaanza kutumika Machi mwakani (2021) kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, ambaye  ameiagiza Manispaa ya Kinondoni  na mkandarasi kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho na maduka 126 katika eneo hilo  unakamilika kabla ya Februari 28, 2021, na kuanza kutumika Machi Mosi.

Kunenge ametoa agizo hilo jana Desemba 16, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali wilayani Kinondoni.

Ameielekeza manispaa ya wilaya hiyo kuhakikisha inampatia mkandarasi fedha kwa wakati ili asipate kikwazo cha kumfanya ashindwe kutekeleza ujenzi huo.

Leave A Reply