Saido Aanza Kuitisha Simba

SUPASTAAmpya wa Yanga, Mrundi, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, amewatisha wapinzani wao, Simba kwa kuwaambia wakikutana uwanjani atapambana kwa ajili ya kufanya vizuri.Saido ameongeza kwamba, licha ya kufunga mabao mawili kwenye mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Yanga, ataendeleza moto wake wa kufunga.

 

Juzi Jumanne, Saido alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Singida United katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Liti, Singida.“Siwezi kusema moja kwa moja ni mechi gani itanisumbua, lakini kila mmoja anajua wapinzani wakubwa wa Yanga ni nani?“

 

Hata hivyo nimepanga kuonesha uwezo na kufanya vizuri kwenye mechi hiyo kwa sababu mapambano bado yapo na yanaendelea,” alimaliza Saido.

Katika hatua nyingine, Kocha mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amesema usajili wa nyota huyo utawasaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza tatizo la kufunga mabao ndani ya kikosi hicho kutokana na uwezo mkubwa wa nyota huyo wa kutengeneza nafasi na kufunga.“

 

Mara nyingi watu wamekuwa wakiwalalamikia washambuliaji wetu kutokana na tatizo la ufungaji, lakini nimekuwa nikisema kwamba kikosi chetu hakina shida ya washambuliaji bali tunakosa watu wanaoweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, ujio wa Saido utatufanya tumalize tatizo hilo.“

 

Licha ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Singida nilichofurahishwa nacho zaidi kutoka kwake ni nafasi za kufunga mabao alizotengeneza kwenye mchezo huo ambapo alitengeneza nafasi zaidi ya nne,” alisema KazeSaidoo anapewa nafasi kubwa ya kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji wikiendi hii kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

STORI: SAID ALLY NA JOEL THOMAS, Dar

Toa comment