The House of Favourite Newspapers

Video: Nyerere Awapiga Mkwara Bongo Fleva

steve-nyerere-1

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Biashara kutoka TSN, Jahu Mohamed (kushoto mwenye suti) akiwakabidhi baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi na Bongo Fleva vifaa mbalimbali vya michezo.

steve-nyerere-2

Wasanii hao wakishikilia vifaa walivyokabidhiwa.

steve-nyerere-3

Msanii wa maigizo hapa Bongo, Steven Mengere ’Steve Nyerere’ (katikati) akizungumzia jinsi walivyojipanga katika mechi hiyo.

steve-nyerere-4

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Biashara TSN, Jahu Mohamed (wa pili kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

steve-nyerere-5

Baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi na Bongo Fleva waliofika kwenye mkutano huo.

Na Denis Mtima/GPL

MSAANII wa maigizo hapa Bongo, Steven Mengere ’Steve Nyerere’, amesema ni lazima watawafunga wasanii wa muziki wa Bongo Fleva katika mechi maalum ya kuchangia fedha kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, hivi karibuni.

Mbali na mechi hiyo, pia kutakuwa na mechi kati ya timu ya soka ya wabunge wa Simba dhidi ya wa Yanga, pamoja na mechi ya netiboli ya Bunge itakayoumana na ile ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Mechi hizo zote zitapigwa Jumapili ya Septemba 25, mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Steve Nyerere ameyasema hayo leoalipozungumza na wanahabari kwenye mkutano uliokuwa umeandaliwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) ambayo ndiyo imedhamini mechi hiyo ya Bongo Muvi dhidi ya Bongo Fleva.

Akizungumza katika mkutano huo,Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Biashara wa TSN, Jahu Mohamed, alisema TSN imejitokeza kudhamini mechi hiyo kutokana na kuguswa na janga hilo na kuona ni vyema kushirikiana na wasanii hao ili kuhamasisha uchangiaji wa pamoja.

Aliongeza kuwa, mbali na kudhamini mchezo huo,pia tayari wametoa mchango ambao tayari wameupeleka kwa waathirika wa tetemeko hilo.

“TSN tunaunganisha nguvu ya wasanii hawa kutoka katika tasnia hizi mbili tofauti kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji wa pamoja,” alisema Jahu.

Katika mchezo huo, viingilio vitakuwa ni Sh 3,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, Sh 10,000 na 15,000 itakuwa kwa ajili ya viti vya rangi ya machungwa huku Sh 50,000, 100,000 na 200,000 ikiwa ni kwa V.I.P C, B na A.

Lakini kwa viti 50 pekee maalum vitakavyokuwa karibu na mgeni rasmi wa mechi hiyo ambaye atatajwa baadaye, kila kimoja kitalilipiwa Sh 1,000,000.

Comments are closed.