The House of Favourite Newspapers

Straika Matata Ataka Sh Milioni 100 Simba

0
Kikosi cha Ruvu Shooting.

NA OMARY MDOSE | CHAMPIONI | HABARI

BAADA ya kuwepo kwa tetesi za Klabu za Simba na Yanga kuanza kumnyatia straika hatari wa timu ya Wajeda, Ruvu Shooting, Abdulrahman Mussa, straika huyo ameibuka na kutaja dau litakalomuondoa klabuni hapo. Mussa msimu huu amekuwa mwiba mkali kwa mabeki wa timu pinzani kutokana na kasi yake ya kuzifumania nyavu ambapo kwa sasa anashika nafasi ya pili kwa ufungaji akiwa na mabao 13 nyuma ya Simon Msuva wa Yanga mwenye 14.

Straika huyo ambaye ndiye Mchezaji Bora kwa Mwezi Aprili, amesema mpaka sasa hajaanza mazungumzo na upande wowote kati ya Simba au Yanga, lakini yupo tayari kuachana na timu yake ya sasa endapo akitimiziwa mahitaji yake kwa timu inayomtaka kwa kumpa kiasi cha Shilingi milioni 100.

“Nimekuwa nikisikia tu kwamba Simba na Yanga zinanitaka lakini bado sijapata taarifa rasmi juu ya hilo labda viongozi wangu ndiyo wanajua kila kitu kuhusu hilo jambo.

“Mimi kwenda Simba au Yanga sina tatizo hata kidogo, nipo tayari kama wakija tukakaa mezani na kukubaliana kila kitu basi nitaihama Ruvu Shooting. “Kwa jinsi nilivyo sasa, thamani yangu inaanzia shilingi milioni 90 mpaka 100, hapo timu ikija na fedha hizo itafanikiwa kunichukua, lakini wakija na pungufu ya hiyo, nitawapa masharti yangu mengine, tukikubaliana nitajiunga na timu yao,” alisema Mussa.

Leave A Reply