The House of Favourite Newspapers

 Straika Simba akubali kutua Coastal

0

MSHAMBULIAJI wa Simba, Charles Ilanfya, amesema kuwa hana pingamizi lolote iwapo uongozi wa klabu hiyo utaamua kumpeleka kwenye kikosi cha Coastal Union kwa mkopo kama ambavyo taarifa zimekuwa zikieleza.

 

Ilanfya aliyejiunga na Simba kwenye dirisha la usajili la Agosti, mwaka huu akitokea KMC, anatajwa kuwa kwenye mipango ya kupelekwa kwa mkopo Coastal ili kupandisha kiwango chake kutokana na kukosa nafasi ya kucheza ndani ya Simba.

 

Tangu ajiunge na Simba, Ilanfya amecheza mchezo mmoja pekee wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons, na amekuwa akipata wakati mgumu kuingia kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ushindani mkubwa wa namba kutoka kwa washambuliaji wengine wa timu hiyo; John Bocco, Meddie Kagere na Chris Mugalu.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, kuhusiana na tetesi za kupelekwa Coastal, Ilanfya alisema: “Kwa upande wangu mpaka sasa ishu ya kwenda Coastal ni taarifa tu ninayoisikia mitandaoni kwani sijapewa ujumbe wowote.

 

“Lakini kuhusu utayari kwangu sina shida, mimi ni mchezaji na naweza kwenda kuchezea timu yoyote itakayonihitaji na kunipa nafasi ya kuonyesha uwezo wangu, iwe Coastal au hata timu nyingine, naweza kwenda kucheza.”

 

Ilanfya msimu uliopita akiwa na KMC alimaliza ligi na mabao sita, kiasi cha kuzishawishi timu za Simba na Yanga kupambania saini yake ambapo Simba waliibuka mabingwa na kumsainisha mkataba wa miaka miwili.

JOEL THOMAS

 

Leave A Reply