The House of Favourite Newspapers

Sven Aidai Simba Mil 102, Aipeleka FIFA

0

Ni miezi mitatu baada ya kuondoka kwenye klabu ya Simba SC, Sven Vandenbroeck ameishtaki klabu hiyo kwa Shirikisho la soka, Fifa kuwa anaidai kiasi cha dola za marekani 44,000 zinazotokana na malimbikizo ya malipo ya ziada.

 

 

Baada ya miezi kadhaa ya kuomba kupewa fedha hizo, Vandenbroeck ambaye sasa ni kocha wa klabu ya AS FAR ya Morocco, ameamua kulipeleka suala hilo kwa Fifa.

 

 

Suala hilo liliripotiwa Fifa majuma matatu yaliyopita na chombo hicho kinachosimamia mchezo wa soka ulimwenguni kimethibitisha kuwa kinafanya uchunguzi kabla ya kufungua kesi.

 

 

Chanzo cha habari kilicho karibu na Mbelgiji huyo kimesema kutopata malipo hayo ni sehemu ya sababu za yeye kuondoka katika klabu hiyo.

 

 

Kuondoka kwake ghafla Simba kuliwaacha wafuatiliaji wa kandanda wa Tanzania na na mshtuko wakijiuliza kwa nini anaondoka baada ya kuwawezesha kufikia hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kwa mara ya tatu katika historia ya Tanzania.

 

 

‘’Kuna sababu nyingi , lakini hasa ni suala la malipo ya tangu msimu uliopita wa mwaka 2019/20. Simba iliahidi mara nyingi kulipa lakini haikufanya hivyo,’’ chanzo hicho kiliuambia mtandao wa PanAfrican Football.

Leave A Reply