The House of Favourite Newspapers

Sven: Vijana Wangu Wakiwa Fiti, Tunashinda Mechi Zote

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji, amesema anafahamu kwamba wanakabiliwa na mechi ngumu za kumaliza msimu huu wa Ligi Kuu Bara, hivyo amekuwa akiomba wachezaji wake wasipate majeraha ili washinde mechi zote.

 

Mbelgiji huyo ameongeza kuwa, kama wachezaji wake wakiendelea kuwa salama, atakuwa na uhakika wa kushinda mechi zao zinazokuja na kuchukua ubingwa wa ligi kuu pamoja na Kombe la FA.

 

“Tunacheza mechi ngumu kwa sasa za kumaliza ligi na utaona bado timu haijawa sawa, tunahitaji muda zaidi wa kuendelea kujifua wakati tunaenda kumaliza mechi zetu.

“Licha ya hivyo, lakini pia nahitaji kuona tunashinda mechi zote zilizosalia na hilo linawezekana kama nyota wangu wote wakiwa wazima.

 

“Pia nataka kuona tunamaliza ligi wachezaji wote wakiwa fiti bila ya kupata majeraha ya namna yoyote ile. Tunapambana kuchukua mataji ya ligi na FA, lakini kitu kikubwa ni kumaliza tukiwa tuko salama kabisa,” alimaliza Sven

STORI: SAID ALLY, Dar es Salaam

KUFURU! USAJILI SIMBA, STRAIKA MGHANA Achota MAMILIONI ya KUTOSHA…

Leave A Reply