The House of Favourite Newspapers

Sweden Yabaini Sehemu Nyingine Ambapo Bomba la Mafuta la Urusi Linavuja

0

Walinzi wa pwani ya Uswidi wamesema kuwa wamegundua sehemu nyingine ya uvujaji wa bomba la gesi la Nord Stream na hivyo kufikisha maeneo manne yaliyo athirika ya miundombinu hiyo muhimu iliyoharibiwa mapema wiki hii kwa madai ya hujuma.

Hapo awali, iliaminika kuwa mabomba hayo yaliyo chini ya Bahari ya Baltic yaliharibiwa katika maeneo matatu, na nyuzi mbili za Nord Stream 1 na Nord Stream 2 zikiathirika.

Lakini msemaji wa walinzi wa pwani ya Uswidi Jenny Larsson aliliambia gazeti la Svenska Dagbladet siku ya Alhamisi kwamba kulikuwa na uvujaji wa nne katika miundombinu hiyo ya chini ya bahari.

“Maeneo mawili kati ya haya yako katika eneo la kipekee la kiuchumi la Uswidi,” Larsson alisema, akiongeza kuwa mengine wawili yalikuwa katika eneo la kipekee la Denmark.

Mamlaka ya Denmark iligundua Jumatatu uvujaji wa mabomba yaliyojengwa ili kupeleka gesi asilia ya Urusi katika nchi za Umoja wa Ulaya, baada ya mtoa huduma huyo kubaini upungufu wa msukumo wa gesi asilia kwenye mabomba ya Nord Stream 1 na Nord Stream 2.

Mamlaka ya Denmark na Uswidi baadaye walisema kulikuwa na mfululizo wa milipuko chini ya bahari karibu na kisiwa cha Bornholm. Hii ilipelekea Urusi, Marekani, na Uswidi kukisia huenda uvujaji huo unaweza kuwa umetokana na kitendo cha makusudi.

Leave A Reply