TAA YA GARI HAIFUNGWI CHUMBANI

PAMBEEEEEE shoga wanakwambia mkaa mkaa tu hata uwekwe ndani ya maji utabaki kuwa mweusi, upo? Utabaki kushangaa wenzako tunapiga hatua kwenye maisha wewe utapiga hatua kwa kutembea, hee heeeiyaaaaa! 

 

Shoga utaishia kuvaa vijora wenzako tunavaa vimini na tunaolewa! Haloooo eeehhhh kweli mseme binadamu ukimsema mnyama utakuwa chizi!

 

Usinione kama nimekuja hivi ukasema ohh Anti Naa leo amekuwa na furaha! Shuuuutuuuuu! Shoga nipo na wewe ambaye huna mbele wala nyuma hakuna kumbi ya starehe ambayo huijui! Najua hili litakugusa maana huna kazi yoyote mjini, kutwa kujua upate danga gani likupeleke viwanja, simu yako imejaa madereva wote wa bajaj na bodaboda, shoga badilika!

Nikisema hivi siku zote huwa namaanisha shoga, haiwezekani mwanamke mwenzangu unakaribia miaka thelathini lakini kutwa kujirahisi mbele ya wanaume, maisha yako yamekuwa ya kuungaunga watoto umekimbiza kijijini kwa mama, inahu?

 

Wajanja wa mjini wanakwambia taa ya gari haifungwi chumbani na siyo kila honi ni gari nyingine ni za baiskeli za kuuza askrimu, upo nyonyo? Kwa nini ujigeuze taa ya gari wakati unajua kabisa ina matumzi yake?

 

Shoga badilika, mwaka ndiyo kwanza bado mbichi, angalia na marafiki wa kuongozana nao siyo kila mtu upo naye wengine wanapotosha na kujikuta ukifika miaka arobaini huna watoto wala mume na maisha yako yanabaki kuwa ya mkatomkato!

 

Kila siku naawaambia sema wanawake wenzangu wengine sijui akili nani anakuwa ametushikia maana leo unasema hili kesho anarudia lilelile! Jamani tubadilike, maisha ya sasa ni magumu na ndiyo maana wanaume wa leo wajanja kama nini, haweza kuoa tu mwanamke ambaye hana mawazo chanya ya kuongoza familia.

Hebu tujiulize, akili zako umezipeleka kwenye viwanja vya starehe, kwenye simu yako una magrupu karibu kumi kutwa kuchati, kwenda kwenye starehe huyo mwanaume gani utampata ambaye anapenda hayo mambo yako?

 

Najua nikimsema sana nyani wakati nimeshika ndizi anaweza kuniparua! Ka leo niishie hapa shoga naona mpaka mate yanataka kunikauka. Tukutane tena wiki ijayo. Ni mimi Anti Naa Shangingi Mstaafu!

Toa comment