The House of Favourite Newspapers

Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation yatoa zawadi za Kompyuta kwa wanafunzi walioshinda baada ya kuandika Insha kuhusu mazingira kwenye maadhimisho ya siku ya tabaka la Ozone

0
Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom  Tanzania Foundation , Sandra Oswald akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 35 ya uhifadhi wa tabaka la Ozone yaliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kufanyika Jijini Dodoma, Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation  ilitoa zawadi za kompyuta  tano zenye thamani ya zaidi ya Tsh.13 milioni kwa ajili ya zawadi kwa  washindi wa kitaifa wa shindano la kuandika Insha kuhusu uhifadhi wa mazingira .
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, George Simbachawene akikabidhi Kompyuta mpakato (Laptops) kwa wanafunzi mbalimbali waliojishindia zawadi kwa kuandika Insha kuhusu uhifadhi wa mazingira wakati wa maadhimisho ya miaka 35 ya uhifadhi wa tabaka la Ozone yaliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kufanyika Jijini Dodoma.
Leave A Reply