The House of Favourite Newspapers

Taasisi za Mafuta za Saudi Arabia Zashambuliwa

0

WAASI wa Houthi nchini Yemen wenye mafungamano na Iran wamerusha ndege 14 zisizo na rubani na makombora 8 katika taasisi za shirika la mafuta linalomilikiwa na serikali ya Saudi Arabia, Saudi Aramco mjini Ras Tanura na katika ngome za kijeshi katika miji ya Dammam, Asir na Jazan nchini Saudi Arabia.

 

Haya yamesemwa jana na msemaji wa kundi hilo la waasi wa Houthi katika kile ambacho serikali ya nchi hiyo imekitaja kuwa shambulio lililotibuka dhidi ya usalama wa nishati duniani.

 

 

Wizara ya nishati ya Saudi Arabia imesema kuwa uwanja wa kuhifadhi mafuta huko Ras Tanura ambalo ni eneo la kusafisha mafuta na kubwa zaidi ulimwenguni la kupakia mafuta pwani, ulishambuliwa na ndege isiyokuwa na rubani iliyotokea upande wa baharini lakini ndege hiyo iliyokuwa na silaha ilinaswa na kuharibiwa kabla ya kufikia lengo lake.

 

 

Katika ujumbe kupitia taarifa msemaji wa wizara hiyo amesema kuwa vitendo kama hivyo havilengi tu taifa hilo la kifalme lakini pia usalama na uthabiti wa kusambazwa kwa bidhaa za nishati duniani na hivyo basi uchumi wa dunia.

Leave A Reply