The House of Favourite Newspapers

Tabasamu Amuombea Kura Shigongo: Kwa Timu Hii, Wamekwisha! – Video

0

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo, jana Ijumaa, Septemba 25, 2020, amezindua rasmi kampeni zake za kunadi sera zake na kuomba kura kwa wananchi wa jimbo hilo ili waweze kumpa ridhaa ya kuwa mbunge kwa miaka mitano ijayo.

 

Akizungumza wakati wa wa kampeni hizo, mgombea ubunge wa Jimbo la Sengerema, Hamisi Tabasamu, alisema: “Hapa tumekuja kuomba kura tatu, za Mheshimiwa Rais, za Shigongo na za madiwani wa CCM.  Mimi nilikuwa diwani wa halmashauri ya Sengerema, tumefanya mambo mengi, kwa mara ya kwanza tunaingiza bungeni timu iliyokamilika na ya kutisha, inakaba mbele na nyuma.  Wamekwisha!

 

“Tunayo miradi mingi na ilani ya uchaguzi imeelezea mengi sana ikiwemo feri mpya na soko letu la samaki, tuna siku chache za kutafuta kura, ni kama siku 35 tu, kura hizi tunazitafuta kijeshi, huu mkutano ulivyoandaliwa ni mkutano wa roho mbaya, hatuwatukani watu wa vyama vingine, lakini wajue CCM imejipanga.

 

“Nitahudhuria vikao viwili, Sengerema na Buchosa, na Shigongo hivyohivyo, tukienda kuomba barabara tunaomba wawili, mimi siendi kuomba uwaziri, nakwenda kutafuta maendeleo kwa wananchi wa Sengerema, naomba ikae vizuri hii.

 

“Dagaa inayovuliwa kwenye Ziwa Victoria katika visiwa vya Wilaya ya Sengerema, tutailinda na itauzwa hapahapa, hatuwezi kupeleka mapato Kirumba.  Hata sisi wananchi wetu ni masikini, muda wa kubembelezana umekwisha,” amesisitiza.

 

Leave A Reply