The House of Favourite Newspapers

Babu (67) Atuhumiwa Kumpa Mimba Mjukuu Wake

0

POLISI mkoani Tabora inamshikilia mzee mwenye umri wa miaka 67, Saidi Abdulatif Tumaini, mkazi wa Kata ya Ng’ambo katika manispaa ya Tabora kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba mjukuu wake mwenye umri wa miaka 13.

 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, ACP Barnabas Mwakalukwa, amesema Novemba 13, mwaka huu, mama mzazi wa mtoto huyo aligundua kuwa binti yake anayesoma darasa la sita Shule ya Msingi Kizigo iliyopo Manispaa ya Tabora ni mjamzito na alipobanwa alimtaja babu yake huyo ambaye pia ni mganga wa kienyeji.

Leave A Reply