The House of Favourite Newspapers

TADB Yawezesha Dhamana Ya Mikopo Ya Sh. 221.3bn/- Kwa Wakulima Wadogo Nchini

0
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB) Kaanael Nnko (kati kati) akiwa katika picha ya pamoja na na Meneja Msimamizi wa Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS) George Nyamrunda (kushoto) na Afisa Biashara Mkuu wa mfuko huo Erasto Sonelo muda mfupi baada ya kumalizika kwa Kongamano la Saba la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linalofanyika jijini Dodoma.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS) imewezesha upatikanaji wa mikopoyenye thamani yabilioni 221.3 kwa wakulima wadogo nchini. 

Akizungumza  wakati wa Kongamano la Saba la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Fedha wa TADB Dkt. Kaanael Nnkoalisema mikopo hiyo iliyotolewa na Taasisi zakifedha washirika wa TADB kupitia mfuko wa SCGS,umewanufaisha wakulima 16,267. 

Dkt. Nnko alieleza kuwa zaidi ya asilima 95 ya wanufaika wa mikopo chini ya mfuko huoni wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo pamoja na wajasiliamali wadogo.

Akielezea mikopo hiyo Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, wanufaika wanawake ni 3,340 ambao wamepatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 16.28 na vijana ni 3,601 waliopatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni  13.6.

Meneja Msimamizi wa Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB) George Nyamrunda (kushoto) akitoa akichangia mada katika kongamano la saba la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linalofanyika jijijini Dodoma. Kulia ni Fatma Kange ambaye ni mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi.

“Maeneo yaliyofikiwa na Mfuko ni Mikoa 27 sawa na alimia 87 ya Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani na Wilaya 123  sawa na asilimia 83 ya Wilaya zote Tanzania Bara na Visiwani,” alisema.

“Mfuko wa SCGS unaosimamiwa na TADB, unasaidia upatikanaji wa dhamana za mikopo ambapo SCGS kwa kushirikiana na taasisi za fedha nchini, inapunguza hatari kwa taasisi hizo ili kuchochea ongezeko la mikopo zaidi kwenye sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambazo ndizo sekta kuu zilizoajiri zaidi ya asilimia 65 ya watanzania wote. Sekta hizi pia zinasaidia upatikanaji wa malighafi za viwandani,” aliongeza.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Saba la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linalofanyika jijijini Dodoma wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) juu ya Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS).

Nnko alisema, Mfuko umechagiza benki kupunguza riba kwa mikopo ya kilimo kwa kuwapatia ukwasi . “Kabla ya kuingia ushirikiano na TADB kupitia mfuko wa SCGS, taasisi za fedha nchini zilikuwa zinatoza riba kati ya asilimia 20 mpaka 36. Lakini, baada ya ushirikiano na kupatiwa ukwasi, benki washirika zimepunguza riba na sasa ni kati ya asilimia 9 mpaka 14 kwa wakulima wadogo. Haya ni mafanikio makubwa ya TADB kupitia mfuko wa SCGS,” alifafanua.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo mpaka sasa TADB kupitia mfuko wa SCGS inashirikiana na taasisi za fedha 16 nchini zenye zaidi ya matawi 700 zikiwemo Benki za Biashara, Benki za Kijamii na Taasisi ndogo za fedha.

Leave A Reply