The House of Favourite Newspapers

Taifa Gas Yaendesha Kampeni Maalumu Ya Matumizi Ya Gesi Wakati Wa Ramadhani

0

Taifa Gas imezindua kampeni maalum wakati wa mwezi wa Ramadhani inayojulikana kama “Ramadhan Iftar Campaign” inayolenga kuhimiza matumizi ya gesi.

Kampeni hii inalenga kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa mkubwa kuhusu matumizi ya nishati ya gesi pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuwafikishia ujumbe Wananchi wake kutumia nishati hiyo.

Timu ya Taifa Gas imetembelea Migahawa kadhaa Jijini Dar es Salaam ikiwemo Mama Land, African Food, Mkongwe Restaurant Kigamboni, Neeko Fast Food Kigamboni, Geza Fast Food Kigamboni Hot Fast Food Sinza ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kampeni hiyo itakayoendelea hadi mwisho wa mfungo wa mfungo.

Afisa Masoko wa Taifa Gas Wilaya ya Kinondoni na Bagamoyo, Arnold Salewa amesema wamewapatia mitungi na zawadi mbalimbali wahusika wa sehemu walizotembelea.

“Moja ya malengo ya kampeni hii ni kuweza kusogeza elimu ya nishati safi na salama kwa ajili ya kupikia, ili kuendeleza juhudi za Serikali na raia wote katika kutunza mazingira yetu kwa ajili yetu sote na vizazi vijavyo.

“Pia lengo lingine ni kuweza kusogeza ufahamu wa bidhaa zetu na kuwaelezea Watanzania wenzetu kwanini Taifa Gas ndio chaguo lao pekee katika matumizi ya nishati Safi na salama. Kwanza bei zetu ni rahisi na huduma zetu ni bora maradufu ukilinganisha na bei tunazouza,” amesema.

Kwa mujibu wa Bw. Salewa, usalama wa mitungi ya Taifa Gas ni wa kiwango kinachokidhi Kimataifa kwani mitungi yote ina valve ya usalama ambayo inapunguza presha ndani ya mtungi pindi inapopanda na kuondoa athari za ajali au milipuko.

“Vilevile tunakufikia hadi nyumbani bure pindi unapotuhitaji kukujazia pia mawakala wetu wanafurahia sana huduma zetu kwani tumesambaa nchi nzima na ndio kampuni pekee yenye vituo vya kujazia nishati kwa Kila mkoa nchini Tanzania.

“Malengo yetu kama Taifa gas ni kuweza kuwafikia watanzania wote nchini Kila nyumba bila kuacha Kijiji Wala mtaa Hadi tutakapotokomeza kabisa matumizi ya Kuni na mkaa kwa manufaa ya nchi yetu na kizazi kijacho.”

Naye, Lulu Mringo ambaye ni Mmiliki wa Mama Land amesema “Nimefurahia kutembelewa na Taifa Gas, kwani tangu nimeanza kutumia gesi zao ni kuwa ina presha kubwa na haiishi haraka na pia wanahudumia wateja kwa haraka.”

Leave A Reply