The House of Favourite Newspapers

Taifa Stars kujipima na Harambee Stars

0

taifa-stars_1.jpg Wachezaji wa timu  ya Tanzania, Taifa Stars.

Na Wilbert Molandi

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepanga kucheza mchezo wa  kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kenya, Harambee Stars Mei 29, mwaka huu jijini Nairobi.

Stars imepanga kutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi yake ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika Juni 04, mwaka huu dhidi ya Misri kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Taifa Stars (2)Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Kenya (FKF) zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki, utakotumika kama sehemu za maandalizi kwa timu zote.

Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na Kocha Mkuu, Charles Mkwasa kinatarajiwa kuingia kambini mwezi ujao, mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Bara ili kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili Misri.

Stars pia itacheza na Nigeria Septemba mwaka huu wakati Kenya inajiandaa na mechi dhidi ya Congo kati ya Juni 3 hadi 5, mwaka huu mchezo wa Kundi E la kufuzu michuano hiyo.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply