The House of Favourite Newspapers

TAIFA STARS WAKWEA PIPA AFCON MISRI, WAAHIDI USHINDI – VIDEO

ibraHiM ajibu wa Yanga, Shomari Kapombe na Jonas Mkude ambao wote ni wachezaji wa Simba, ni miongoni mwa wachezaji walioachwa kwenye msafara wa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kinachoenda kuweka kambi nchini Misri kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Mataifa afrika (afcon) nchini humo.

Taifa Stars ikiwa imepangwa Kundi C na timu za Kenya, Senegal na Algeria, ikiwa kambini itacheza mechi ya kirafiki na wenyeji wao, Misri. Wengine walioenguliwa kwenye msafara huo ni Kennedy Wilson wa Singida United, Ally Ally (KMC), Khamis Khamis (Kagera Sugar) na Ayoub Lyanga (Coastal Unon).

 

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike amesema: “Mchujo umefanyika mazoezini, nidhamu na kujituma ni sehemu ya vigezo ambavyo vimetumika. “Ukiwa mazoezini unaona namna mchezaji anavyojituma, hicho ndicho kimepelekea uwepo wa mchujo na kupatikana nyota hawa.”

Taifa Stars imeenda Misri na wachezaji 32, kisha baadaye utafanyika mchujo mwingine na kubaki nyota 23 pekee ambao ndiyo watashiriki Afcon. Tisa watakaobaki wataendelea kukaa kambini kwa maandalizi ya michuano ya Chan inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

 

Kikosi hicho cha nyota 32 ni makipa; Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Mbao FC), Suleiman Salula (Malindi SC) na Aaron Lulambo (Tanzania Prisons). Mabeki; Claryo Boniface (U20), Hassan Kessy (Nkana FC, Zambia), Vincent Philipo (Mbao FC), Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’, Erasto Nyoni (wote Simba SC), Kelvin Yondani, Gardiel Michael (wote Yanga SC), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Ally Mtoni (Lipuli FC), David Mwantika na Aggrey Morris (wote Azam FC).

Viungo; Feisal Salum (Yanga), Himid Mao (Petrojet, Misri), Frank Domayo, Mudathir Yahya (wote Azam FC), Shiza Kichuya (ENNPI, Misri), Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadidi Morocco), Farid Mussa (Tenerife, Hispania) na Freddy Tangalu (Lipuli FC).

Washambuliaji; Yahya Zayd (Ismailia, Misri), Shaaban Iddi Chilunda (Tenerife, Hispania), Rashid Mandawa (BDF, Botswana), Miraj Athumani (Lipuli FC), Kelvin John (U17), Adi Yussuf (Solihull Moors, England), John Bocco (Simba SC), Thomas Ulimwengu (JS Saoura, Algeria) na Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji).

 

Juni 23, mwaka huu, Taifa Stars itaanza Afcon kwa kucheza na Senegal, kisha Juni 27 dhidi ya Kenya na kumaliza hatua ya makundi Julai Mosi dhidi ya Algeria.

Comments are closed.