The House of Favourite Newspapers

Taifa Stars Yaondolewa Mbio za Kuelekea CHAN, Yaambulia Kipigo Kingine Uganda

0

 

Mohamed Hussein akiwa katika mechi

TIMU ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeambulia kipigo kingine cha pili dhidi ya Uganda cha mabao 3-0 katika dimba la St Mary’s na kuondolewa rasmi katika mbio za kushiriki mashindano ya CHAN mwakani nchini Algeria.

 

Hadi mapumziko Stars ilikuwa imesharuhusu bao moja bila kwa mkwaju wa penati baada ya Jonas Mkude kumchezea madhambi mchezaji wa Uganda ndani ya eneo la hatari.

 

 

Katika mchezo wa awali uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Timu ya Taifa ya Uganda iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

 

Leave A Reply