The House of Favourite Newspapers

Watu 18 Wauawa na Magari Kuchomwa Moto katika Shambulio la Al shabab Nchini Somalia

0
Magari yaliyochomwa moto katika shambulio

WATU 18 wameuawa na kikundi cha Al Shabab ikiwa ni pamoja na kuchoma chakula kilichokuwa kinapelekwa katika Mji wa Mahan ambao unakabiliwa na upungufu wa chakula baada ya kuwa na mapigano ya mara kwa mara yanayotekelezwa na Al Shabab wenyewe.

 

Vyombo ya Habari ya nchini humo vimeripoti kuwa wapiganaji hao wa Al Shabab walichoma moto magari yaliyokuwa yamebeba chakula na kusababisha vifo vya watu waliokuwemo ndani ya magari hayo.

Al Shabaab wanataka kuitawala Somalia kwa sheria za Kiislamu

“Al Shabab wameua watu 18 pamoja na kuchoma magari yaliyokuwa yamebeba chakula kuelekea mji wa Mahas.” amesema Kiongozi wa eneo hilo Farah Aden.

 

Kikundi hicho ambacho kinahusishwa na kundi la kigaidi la Al Qaeda limekuwa likipambana na Serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 10 likitaka kutengeneza utawala wake ambao utakuwa ukiendeshwa kwa misingi ya dola ya Kiislam

 

 

Leave A Reply