The House of Favourite Newspapers

Taifa Stars Yapigwa Bao 3-0 na Cape Verde Mjini Praia

Taifa Stars imekukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Cape Verde katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Capo, Mjini Praia.

Mabao  ya Cape Verde  mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Ricardo Gomes kabla ya Yanique Tavares kuhitimisha kwa bao tatu.

 

 

Mshambuliaji wao, Ricardo Gomes anayekipiga nchini Serbia katika klabu ya Rartizan ndiye alipachika mabao hayo katika dakika ya 16 na 23 akitumia vizuri uzembe wa mabeki wa Stars, David Mwantika na Hassan Kessy, kabla ya Tavares kumalizia la tatu dakika ya 84 kwa shambulizi la kushtukiza.

 

Washambuliaji Stars wakiongozwa na nahodha Mbwana Samatta walishindwa kabisa kutumia nafasi chache walizopata kupata mabao.

 

Kutokana na matokeo hayo, Cape Verde inapanda mpaka nafasi ya kwanza ya Kundi L iliyokuwa inakaliwa na Uganda ‘The Cranes’ kwa kuwa na idadi kubwa ya mabao, Lesotho ya tatu na Taifa Stars inashika mkia.

 

Cape Verde na Uganda wana idadi ya pointi sawa ambazo ni nne. Uganda watacheza mchezo wao wa tatu kesho Jumamosi na Lesotho.

 

Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano na Cape Verde Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Taifa Stars:
Aishi Manula, Hassan Kessy, Gadiel Michael/ Shomari Kapombe, David Mwantika/ Ally Sonso, Agrey Morris, Abdi Banda, Himid Mao, Mudathir Yahya/ John Bocco, Simon Msuva, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu
Matokeo mengine ya mechi

Cameroon 1 – 0 Malawi
Gabon 3 – 0 Sudan Kusini
Togo 1 – 1 Gambia
Guinea 2 – 0 Rwanda

Comments are closed.