TAKUKURU YAAHIDI ZAWADI ATAKAYESAIDIA KUPATIKANA HANS POPE – VIDEO

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) imewataka aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope na Frankline Lauwo kujisalimisha katika ofisi zake au kituo cha polisi kujibu tuhuma zinazowakabili.

 

Aidha, TAKUKURU imetangaza zawadi nono kwa mwananchi atakayefanikisha kupatikana kwa Hans Pope na  Lauwo baada ya TAKUKURU kuwatafuta kwa njia za kawaida bila mafanikio.

 

Katika kesi hiyo, ambayo inayowahusisha pia kina aliyekuwa Rais wa Simba, Evance Aveva na katibu wake, Geofrey Nyange “Kaburu”, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwa TRA juu ya ununuzi wa nyasi bandia za Uwanja wa Simba SC.

Loading...

Toa comment